HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde
amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi
277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na
wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde
amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu
ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka
2015.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu,
amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu
ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.
Kwa upande wa masomo, amesema
ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic
Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya
asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililoongoza kwa ufaulu ni
Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths
ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Kati ya wanafunzi 10 bora
kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri
kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam
Kati ya shule 10 zilizofanya
vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule
iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora
kitaifa, hakuna shule ya serikali
Mkoa wa Njombe umeongoza katika
mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma
na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na
Wang’ing’ombe pia zikiibuka vinara.
BOFYA HAPA KUANGALIA
No comments:
Post a Comment