Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Tuesday, January 31, 2017

NAFASI ZA AJIRA SERIKALINI LABARATORY TECHNICIANS

NAFASI ZA AJIRA SERIKALINI LABARATORY TECHNICIAN
Serikali inatarajia kuajiri Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule Daraja la II. Ajira hii ni kwa Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule waliohitimu kati ya mwaka 2013 - 2015.
 Hivyo, wenye sifa stahiki na wanaotaka kuajiriwa Serikalini, wanatangaziwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya:
  • Elimu ya Sekondari (Kidato cha nne na / au Sita);
  • Taaluma ya Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule na
  • Cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya uhakiki.
Aidha, mwombaji aambatishe nakala ya wasifu binafsi (CV) ya Elimu, Taaluma na Uzoefu.  Mwombaji aainishe majina yake matatu kwa kirefu na usahihi.
Mwombaji ambaye katika vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha IV au Kidato cha VI katika masomo ya Sayansi na waliofuzu Mafunzo ya Laboratory Technology au Laboratory Science and Technology katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kupata Stashahada (National Technical Awards [NTA] Level VI) au Full Technician Certificate.
KAZI ZA KUFANYA
  1. Kutayarisha vitendea kazi vya maabara ya somo la Sayansi kwa vitendo.
  2. Kusaidiana na mwalimu wa somo katika kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo.
  3. Kupokea na kutunza vifaa na madawa kwa ajili ya maabara ya shule.
  4. Kubaini mahitaji ya vifaa na madawa kwa ajili ya maabara ya shule.
  5. Kufanya majaribio ya awali (Pre-Test) kabla ya majaribio (Practical) kufanyika na wanafunzi kwa mazoezi na mitihani ya ndani.
  6. Kutunza vitendea kazi na kuhakikisha usafi wa maabara kabla na baada ya mazoezi ya mitihani na majaribio ya ndani.
  7. Kusimamia usalama wa maabara na waliomo wakati wa mazoezi ya vitendo (Practicals) kwa kuhakikisha kuwepo vizimamoto (Fire Extinguisher).
  8. Kutunza vifaa vya usalama na huduma ya kwanza kwenye vyumba vya maabara.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti / nyaraka halisi na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘file’ moja la ‘pdf’.  ‘File’ lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
  2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
  1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 20 Februari, 2017.
  2. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira
  3. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
IMETOLEWA NA
Tarishi M.K.
KATIBU MKUU
30 Januari 2017

No comments:

Post a Comment