Fanya Yafuatayo Ili Kuhamia Mtandao Mwingine Bila Kubadilisha Namba
Mobile Number Portability (MNP)
Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe
01 Machi 2017.
Huduma ya MNP ina faida zipi?
Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe
01 Machi 2017.
• Utaendelea kutumia namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine na hivyo kufurahia uhuru na huduma za mtoa huduma
mpya.
• Utapokea simu na meseji bila kujali ni mtandao upi umehamia na bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika katika shughuli zako kwamba umebadilisha mtoa huduma wako.
• Utaokoa fedha kwa kuwa hutakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja.
• Utaweza kuchagua mtoa huduma ambaye unaona
anatoa huduma bora zaidi, anakidhi matarajio yako na
ana ubunifu katika kutoa huduma.
Ni Nini Unatakiwa Kufanya Ili Kupata Huduma Hii?
1. Nenda vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa huduma unakotaka kuhamia na umueleze mhudumu kwamba ungependa
kuhama na namba yako.
2. Mhudumu atakutaka ujaze fomu maalum ya maombi (fomu moja).
3. Sehemu ya Fomu ya maombi ya kuhama ni tamko rasmi kwamba unakubali kuwa utawajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma ulizokuwa unapata kutoka kwa mtoa huduma wako wa awali kama yapo.
4. Utatakiwa kutoa vitu vifuatavyo: –
a) Kitambulisho chenye picha yako – kinaweza kuwa Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.
b) Simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba unayotaka kubaki nayo.
5. Iwapo una salio katika akaunti ya pesa mtandao utashauriwa kutoa pesa kabla ya kuhama.
6. Utatakiwa kutuma meseji yenye neno “HAMA” kwenda namba ‘15080’ ambayo ni namba maalum ya kuhama.
7. Utapokea meseji kukujulisha kwamba maombi yako yamepokelewa.
8. Iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na sababu mbalimbali ikiwapo madeni maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa meseji kuhusu maendeleo ya mchakato huu.
9. Mtoa huduma wako mpya wa huduma za simu za kiganjaji atakupatia laini mpya.
10. Ili kuzuia kupokea mihamala ya fedha mtandao wakati wa kuhama, huduma za kifedha zitasitishwa kwa muda mpaka namba ikapohamishwa kwa mtoa huduma mpya.
11. Katika hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka, iwapo utachelewa si zaidi ya saa 48. Utatumiwa ujumbe mfupi kuwa uhamaji umekamilika na ubadilishe laini.
12. Ikifikia hapo, weka laini mpya uliyopewa na mtoa huduma wako mpya kwenye simu yako. Iwapo huna uhakika wa nini cha kufanya, unaweza kwenda kwa mtoa huduma wako mpya au wakala wake au kuwapigia simu na wataweza kukusaidia.
13. Mchakato umekamilika.
Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe 01 Machi 2017.
Kwa Maelezo Zaidi Piga 0222 100 100 Au Tembelea Tovuti Ya TTCL TANZANIA
No comments:
Post a Comment