Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Monday, February 20, 2017

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NECTA SHARE NA KWA RAFIKI ZAKO

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA

Baraza la Mitihani la Tanzania limesikitishwa na taarifa ya UONGO iliyotolewa na Gazeti la Nipashe toleo Na. 0579130 la tarehe 19 Februari 2017 yenye kichwa cha habari kilichosomeka Mchujo FORM 1 Wasisitizwa. Katika taarifa hiyo mwandishi aliuarifu umma kuwa Katibu Mtendaji amesisitiza uwepo wa Upimaji huo na kwamba umeshapitishwa. Baraza linapenda kuwajulisha wanafunzi na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.

Hivyo,Baraza    linaomba    umma     kuzipuuza   taarifa     hizo    kwa     kuwa    upimaji    huo
ULISHASITISHWA na HAUTAKUWEPO.
 
 
Imetolewana,


AFISA HABARI NA UHUSIANO

No comments:

Post a Comment