Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Tuesday, March 14, 2017

FUATILIA RIWAYA HII YA NANI WA KUNIFARIJI? BY ERICK NGABO SHARE KWA RAFIKI ZAKO

Sehemu ya I ya

NANI WA KUNIFARIJI? imetungwa

Na Erick@NGABO


Ilikuwa jioni yenye sifa zake maalum :mawingu yalikuwa mekundu huku sehemu ndogo ikionekana na bluu , mama yake Alifika nyumbani na kusalimiwa na mtoto kifunga mimba:
"Shikamoo mama!"
"Marahaba mwanangu!"
Mama," habari za jioni na majukumu ya kazi?"
Ni kama nzuri mwanangu!!
Mama alionekana kuwa na mchoko mkubwa na moyo wenye kusongwa na mawazo , akazitua kuni alizokuwa nazo pia akatua na dumu alilobeba mkononi likijaa maji.
Hakujua ni nini kilichokuwa kinamkosesha raha na japo wanasema "raha jipe mwenyewe"alijitahidi kujikiwaza bila mafanikio.
Aliingia jikoni huku akitafuta chungu cha kupikia viazi mviringo akawa haoni sababu ya kukikosa.
Akamwita mwanae ili amwulize kama huenda wamekitumia mchana ndipo mtoto kasema:"
Mama si hicho karibu na miguu yako!!"
"Mungu wangu wee" mama alishangaa . Ni kweli maskini hana likizo.
Alipika chakula kikawa tayari na kuitandika meza yake usiku huku akimsubiri mumewe .
Ghafla mume wake alifika kutoka kazini ila akatambua kuwa hali ya mkewe si nzuri .
Alikaribishwa mezani lakini hakuwa na hamu ya chakula wakati huo ila alijitahidi kula kwa maana kwamba angemliza mkewe. Baada ya chakula, alijirusha moja kwa moja kitandani ika mama-watoto alikaa sebuleni na kutafakari:
" Mungu ndiye mweza wa yote, hana upendeleo , aweza kuniokoa ktk hali hii ya huzuni ambayo sioni sababu yake.Eti penye nia pana njia , nikijipa moyo huenda hayo yakafikia kikomo.
Mtoto wangu aliondika kwenda mjini kuna miaka kumi , nilikuwa nampenda sana ,alikuwa mwenye bidii , hakuwa na ubaya wowote lakini Mungu uliona vema apitie njia ile, sijui kwamba yuko hai au kama huenda aliliwa na mazimwi maana mjini kuna mengi.
Inawezekana alioa au kuuawa na majambazi pengine huenda ...."
Katika fikira hizo hizo alizokuwa nazo kuhusu mtoto wake kifungua -mimba jina lake TAABU , aliivuta pumzi kisha akaenda kitandani.
Punde si punde alianza kuweweseka kama anayepigwa na majambazi ndotoni kisha.......

JIUNGE NAMI KTK SEHEMU YA II

No comments:

Post a Comment