Tangazo kwa madaktari wa Tanzania kwenda kufanya kazi Kenya
*JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*
*WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WAZEE NA WATOTO*
*TANGAZO LA KAZI KWA MADAKTARI*
WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA WAZEE NA WATOTO WANAPENDA KUWAARIFU WANANCHI KUWA *SERIKALI YA KENYA* INA MAFASI 500 ZA AJIRA ZA MKATABA KWA MADAKTARI WATANZANIA WENYE SIFA AMBAO WANGEPENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA WATUME MAOMBI YAO KWA NJIA YA BARUA PEPE AMBAYO NI maombiyakazi@moh.go.tz KABLA YA *TAREHE 27 MACHI SAA 10:00 JIONI* BAADA YA HAPO MAOMBI HAYATAPOKELEWA
MAOMBI YAAMBATANISHWE NA NYARAKA ZIFUATAZO
1.WASIFU (CV) YA MWOMBAJI
2.NAKALA ZA VYETI VYA TAALUMA
3. TRANSCRIPT
4 NAKALA YA CHETI CHA KUZALIWA
5.CHETI CHA KUHITIMU INTERNSHIP
6.NAKALA YA CHETI CHA USAJILI KUTOKA BARAZA LA MADAKTARI LA TANGANYIKA
NB: *PAMOJA NA NYARAKA ZILIZOTAJWA HAPO JUU ,MUOMBAJI ANATAKIWA KUJAZA JEDWALI LILILOAMBATANISHWA NA TANGAZO HILI KATIKA MFUMO WA EXCEL*
*TANGAZO HILI HALIWAHUSU* WATUMISHI WA UMMA ,HOSPITALI TEULE ZA HALMASHAURI NA HOSPTALI ZA MASHIRIKA YA HIARI AMBAO WANALIPWA MSHAHARA NA SERIKALI.
WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA WANATARAJIWA KUPEWA MKATABA WA AJIRA MIAKA MIWILI(2)
*IMETOLEWA NA:*
Katibu Mkuu (Afya)
Wizara Ya Afya ,Maendeleo Ya Jamii ,Jinsia Wazee Na Watoto
DODOMA
18 MACHI,2017
Katibu Mkuu (Afya)
Wizara Ya Afya ,Maendeleo Ya Jamii ,Jinsia Wazee Na Watoto
DODOMA
18 MACHI,2017
No comments:
Post a Comment