Mama aliwashukuru sana kumkaribisha vizuri kiasi kile kisha akawakaribisha mezani wakala chamcha pamoja.
Aliletewa taulo la buluu akaingia bafuni kuoga, aliyafurahia maji kiasi kwamba aliyafunga na kuyafungua kwa muda na kutazama yanavyodondoka...ilikuwa ni tofauti kubwa sana na pale alipokuwa kijijini kwao alikozoea maji ya mtoni tu.
"Faraja! Hujamaliza?"
Bosi wake alimwita kwa sauti.
"Naam mama , tayari ninakuja " Faraja alijibu kwa sauti ya upole.
Aliambiwa kuwa kazi yake ya kila siku ni kupika akasema kuwa haiwezi kwa sababu hakujua kupika isipokuwa viazi na maharage tu!!
"Usijali nitakupa jinsi" Kesho asubuhi nitakupeleka mahali ambapo watakufundisha wiki mbili mfululizo utakuwa umeshajua vizuri."Bosi alimimwambia.
Faraja:"Asante mama"
"Ahadi ni deni" Mama alijiambia moyoni na kuamka asubuhi mapema akamwamsha Faraja wakanywa chai kisha wakaenda moja kwa moja eneo la kufundishiwa .
Mama alikuwa anampeleka Faraja kila siku mpaka pale alipojua kupika vizuri .
Siku moja Mama yule alimwambia Faraja kuwa ni yeye wa kuandaa mchuzi, mayai ya kukaangwa na chipsi za ndizi .
Faraja alikubali bila shingo upande .
Kabla ya hapo ,Alikuwa anafikiri kama atathubutu kumwambia Yule mama kuwa ameweza ama kweli "Penye nia pana njia!"Alijikaza na kuanza kuanda alivyoamuriwa na Yule mama Bosi wake!
Siku hiyo aliandaa kila kitu kwa umakini na ujuzi mwingi sana ungefikiri ana udhamiri ktk upishi kumbe si alifundishwa wiki mbili tu!!
Aliweka chakula mezani na kadri muda wa kufika kwa Mama yule Bosi wake ulivyokuwa unakaribia ndivyo Faraja alivyozidi kufikiri kuhusu chakula alichokiandaa.
"Biiii" Honi ya gari la Bosi wake ilisikika na punde si punde mlinzi alimfungulia Mama yule.
Baada ya kutoka bafuni, walikaribishwa mezani na kula chakula kwa pamoja!!
"Aisee Faraja nani kapika chakula kitamu kiasi hiki?
"Ni mimi mwenyewe"Bahati alijibu kwa tabasamu.
"Hongera sana mwanangu!'
"Asante mama"
Bahati aliendelea kuwa na ufanisi mkubwa ktk kila jambo na mpaka habari zake za kikazi zikaenea katika mji mzima!
Alikuwa nashahara mzuri akiokuwa anapewa kwa muda naye akikuwa anatunza hela yake vizuri.
Alifanya kazi ya kupika miaka mitatu watu matajiri,wabunge na hata mawaziri wakaanza kumtamani eti awe mpishi wao ila hakukubali kamwe maana alikua alikotoka na yule mama Bosi wake ambaye alimwongezea mshahara aliposikia taarifa hizo kuwa wanamtamani wengine .
Ikumbukwe kuwa Faraja alihamia mjini huku akiwa na lengo moja maalum la kuhamia nchi za kigeni.
Alikusanya hela yake yote akaanza kutafakari jinsi atakavyomuaga yule mama Bosi wake.
"Sitamwambia uongo , najua ataniruhusu na kama la hakubali nitavumilia mpaka pale atakapokubali."FARAJA alijiambia moyoni.
Alipothubutu kumwomba ruhusa ya kutoka akamruhusu bila tatizo akasema kuwa kwa namna alivyokuwa mnyenyekevu ,mpole na na mpenda-kazi, atamzidisha laki moja ya zawadi kwa tabia alioionyesha.
Alimsaidia kujiandaa na akamsindikiza kwenda kituoni pa mabasi mama akijua anaenda nyumbani alimwambia
:" kwa heri, safari njema pia uwasalimie wazazi wako wote!"
"Kwa heri Mama pia asante sana kwa ushirikiano mzuri !God bless " Faraja alijibu.
Walitazamana machoni na kuagana kwa busu kisha machozi yakatililika kwa jinsi mama alivyokuwa anampenda sana Faraja.
Faraja akaanza safari kwenda nchi nyingine .
TUKUTANE SEHEMU YA TANO
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment