Sehemu ya II :
Punde si punde alianza kuweweseka kama anayepigwa na majambazi ndotoni ndipo mumewe kamshitua na kumwuliza kwa mshangao : "Umekuwa wapi kipenzi?" "Aaah sijui kwani kulikoni?" Mkewe aliuliza. Kwa sababu ilikuwa katika usiku wa manane ,wote walipatwa na usingizi wakasinzia japokuwa upande wa mke ulikuwa usingizi wa mang'amung'amu Yaani mara alisinzia mara alishituka. Kesho yake asubuhi waliamka na kwenza kazini zake kila mmoja. Mama aliporudi akafika nyumbani akiwa ametulia tuli kama maji mtungini. Papo hapo akausikia mlio wa mtu apigaye mlangoni : "Hodi hapa!' "Karibu sana tupo!" Mama-watoto alufurahi kumpokea HURUMA, mgeni wa mtaa mmoja na shemeji yake. Akamkaribisha sebuleni na kuongea naye kwa muda: *Humm vipi habari za siku nyingi, shemeji yangu hajambo? *Hajambo pia nimekuja hapa kwa sababu amenituma nije kukuona kwamba ana jipya la kukwambia. *Jipya lipi jameni? *Fara.. .Ja ..... *Faraja nani...kafanya nini....? *FARAJA mwanawe amempigia simu shemeji yako na kumwachia ujumbe maalum kwa niaba yako . *Daaah, Mungu wangu weee ama kweli nimepoteza fahamu na huenda niko ktk dunia nyingine!!! Alimkumbatia mgeni huku akiwa na furaha tele moyoni pia uso wake ulikuwa mithili ya kibogoyo anayeota meno. Mama Faraja nimesahau , shemeji yako kaniambia kuwa ikiwezekana uje twende kumwona pamoja. Bila shaka usijali. Wakatoka nje na kuifuata njia ya kuelekea kwa shemeji yake . Wakiwa karibu na lango ,walipakutania na mumewe yaani Baba Faraja akamwuliza : ⛷Mnaenda wapi mama?? Ninaenda kwa shemeji sikawii maana ana ujumbe maalum kutoka kwa faraja mume wangu!! Hummmm!!sauti ya dharau ilisikika kutoka kwa mumewe alipogeuka kumwangalia akamwona amekunja uso mfano wa aliyepoteza hundi ya benki ya milioni 10. Akafikiri ni kwa sababu ya mchoko wa kazi maana mumewe alikuwa na kazi nzito sana. Mume alitembea polepole huku akiwa na msongo mkubwa wa mawazo : Faraja angali hai?? Au ni zimwi lake?? Siamini hilo ila...pia... ? Hayo ni baadhi ya maswahili kahaa aliyojiuliza asipate jibu. Alianza kukumbuka alivyomkosea mwanawe alipokuwa na umri wa miaka 20 kwamba atamwuua, alivyokuwa anampiga na kumwambia :"ukimwambia kwamba nimekupiga nitakukata kichwa!!" Alikumbuka pia alivyomtishia kuwa asipokubali kurithi uchawi na mahirizi ya marehemu bibi yake atamezwa na mazimwi. Mwisho kabisa alikumbuka siku alipokuwa na Faraja chumbani bila ya mama yake Faraja kuwepo , akaanza kumbembeleza arithi vya bibi , Faraja akakataa , baba yake akawaita na akawatuma mijusi, vinyonganyonga,konokono,jongoo ... Wakajaa kwenye mkeka ule waliokalia ungesema ni mchanga baharini . "Mama, mama, mama!!!" Mtoto alilia akimwita mamaye lakini hakuwepo. Kubali kurithi usife , mtoto kakataa katakata. Baba kamwambia "Toka hapa kama hutaki kufa, pumbavu mkubwa wewe! Mtoto katoka nje kwa kutoroka mithili ya mbuzi wanaoachiwa kutoka zizini baada ya siku 5 bila kwenda malishoni. Huo ukawa mwanzo wa uamuzi wake kwenda nchi ya mbali kuogopa kifo, kuliwa na mazimwi n.k Alienda bila kumuaga yeyote yule hata ndugu wala mama yake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
JIUNGE NAMI Ktk SEHEMU YA III
No comments:
Post a Comment