Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Wednesday, March 15, 2017

NANI WAKUNIFARIJI SEHEMU YA TATU(3) SHARE KWA RAFIKI ZAKO

Karibuni katika sehemu ya III ya NANI WA KUNIFARIJI?
Imetungwa nami ERICK @NGABO
FARAJA mtoto kifungua -mimba aliamua kwenda nchi ya mbali kutokana na takwa la baba yake eti arithi uchawi wa bibi yake.

Siku ile alimtoroka baba yake wakiwa chumbani , aliamua kwenda mtaa mwingine kwa rafiki yake waliosoma sekondari pamoja .
Baada ya kukaribishwa aliwaambia kuwa anatangulia kulala kwao kwa sababu ya safari.
Hakuulizwa safari ya wapi ila alitandikiwa kitanda akajinyosha mithili ya mtu aliyechoka sana.
"Wee YOHANa!!" kwa heri tutaonana Mungu akipenda, unajua wewe ni rafiki yangu wa dhati uwe unanikumbuka tena katika maombi yako .
YOHANA: Hummm !!Alijishitua na kusema :"Mbona unaenda usiku? Faraja akasema :sina woga kwa heri Baba!!
Wakapeana mikono na kuambatana mpaka mlangoni ili amfungulie pia akawaaga wazazi wa Yohana papo hapo.


Ndege walianza kulia, umande uliomfunga machoni mfano watu avaaye miwani ya jua ulimfanya ahuzunike zaidi .
"Haya yote ni kwa sababu ya babangu asingelinilazimisha urithi nisingeli Pata taabu kiasi hiki!" FARAJA aliwaza moyoni.

Safari yake Faraja kwenda mji mkuu wa nchi yao kutafuta maisha huku akimkimbia babake ilikuwa nzito kama kubeba kg 100 za mawe na zege kichwani: alilala porini, alikula matunda na majani mabichi kama ng'ombe maana nchi yao watu walikuwa katika vijiji sana lilihali naye hakupenda watu wamwone.
Baada ya wiki moja alifika mjini na alipofika mjini akabahatika kuokota franga laki 4 , alifurahi na kuanza kuyasahau ya kijijini.
Ama kweli "ng,ombe wa maskini hazai na hata akizaa huzaa tasa!" Faraja alilala katika mfereji bahati mbaya majambazi wakamvamia na kumpora zile laki 4 zote , pale pale alipigwa kishenzi lakini akajikaza kisabuni hakulia!!

Asubuhi mapema aliamka na kuanza kuuona mwanga wa mjini ,majumba na maghorofa ya rangi mbalimbali ila hakufurahishwa navyo kamwe kwa sababu ya majambazi waliomvamia jana usiku.
Alikumbuka methali "Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo" akafungua mdomo na kusema baada ya dhiki ni faraja , akatanguliza mguu wake wa kulia kwenda mbele.

"Nipate maji wapi , nipate choo wapi?"
Alijitwika nira na kujikaza kiume ndipo akakumbuka wimbo wa utotoni:
"Silie mama ,silie baba Maisha ni duara pia ni kama maua ,mara yanayauka mara yako sawa."

Baadha ya saa 5 alikutana na limama likubwa lilokuwa ndani ya bajaji , lilipomwangalia alivyokuwa anachechemea likamwamuru mwendesha bajaji asimame karibu naye.

FARAJA: shikamoo mama mheshimiwa!! Alimwamkia kwa sauti ya huruma!
MAMA: marahaba mwanangu!
Mbona unachoka sana pia wewe mgeni humu mjini una haja ipi?
FARAJA: Ninatoka ....aliogopa kusema anakotoka.
Mama sina kazi pia niko mgeni humu mjini ni kweli!! Unataka kazi gani?
Mama kiukweli kazi yoyote ile naweza kuifanya!! 'Karibu sana kwangu nina kazi ya kufanya ... "
Mama alimkaribisha wakakaa naye ndani ya bajaji kwenda nyumbani .
"Nimekupenda mwanamgu usijali" Mama aliongea kwa tabasamu.
"Asante mama" Faraja alishukuru kwa furaha tele huku uso wake uking'ang'aa mfano wa theluji.
Kumbe limama lile lilimpenda kwa sababu Faraja alikuwa na sur a kama ya Mwanawe kifungua-mimba.

"Haya mama chukua chenji yako niwahi mjini kuna mteja naenda kupelekea watoto!!"Mwendesha-bajaji alisema
"Haya baba, asante pia safari njema"

Mama alijibu .
"Karibu sana Mwanangu , kochi hapo kaa upumzike!!
"Ama kweli siku njema huonekana asubuhi"
Faraja alianza kuwaza moyoni na pale alipo kuwa anawaza hayo watoto wote wakaababatana na mama yao kuja kumsalimia Faraja!!
"Hujambo mgeni wetu!!
"Sijambo sana, nanyi hamjambo?"
"Hatujambo sana pia karibu kwetu jisikie huru!!"
Mama aliwashukuru watoto kumkaribisha Vizuri sana kiasi kile kisha akawakaribisha mezani wakala chamcha pamoja.

Jiunge nami katika sehemu ya 4


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment