Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Saturday, March 25, 2017

WANAFUNZI WOTE TANZANIA KUPIMWA TB KWA LAZIMA




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku shule za binafsi na serikali kupokea wanafunzi bila kupimwa ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB)
Pia Waziri Ummy ameagiza watu walio katika makundi hatarishi wakiwemo wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI na wajawazito wafike vituo vya Afya kupimwa Kifua Kikuu (TB).






Akitoa maagizo hayo leo Jijini Arusha kwenye maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani, Ummy alisema lengo la kupima makundi hayo muhimu ni kuzika kuenea kwa ugonjwa huo mapema, kwani mgonjwa mmoja ana uwezo wa kuambukiza watu 20 kwa mwaka kama hajaanza kutumia dawa kitu ambacho ni hatari.

"Makundi hatarishi ambayo lazima wapimwe wale wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, watoto chini ya miaka mkutano, wajawazito, wafungwa, watumiaji madawa ya kulevya, watu wanaougua saratani na kisukari lazima wapime Kifua Kikuu kwa lazima," amesema
Alisema tatizo ni kubwa nchini kwani takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Tanzania kwa mwaka 2015 jumla ya watu 160,000 waliugua Kifua Kikuu kati ya hao watu 62,180 sawa na asilimia 39 tu ndiyo waligunduliwa na kupata matibabu.


"Hii inamaanisha katika kila watu 100,000, watu 306 wanaougua ugonjwa wa Kifua Kikuu kila mwaka nchini na kati ya hao wanaougua inakadiriwa watu 55,000 wanafariki dunia kila mwaka," amesema
Amesema Mkoa wa Dar esalaam bado unaongoza kuwa na idadi kubwa yawagonjwa wa kifua kikuu ambapo waliopo ni asilimia 22, ikifuatiwa na Mwanza, Mbeya, Morogoro, Shinyanga, Arusha, Mara, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
"Mikoa hii pamoja na Daresalaam huchangia asilimia 63 ya wagonjwa wote waliogundulika nchini mwaka 2015," amesema
Amesema kutokana na hilo serikali imeweka mkakati kuongeza vituo vyenye mashine za kisasa za kupima kifua kikuu kutoka mashine 70 hadi kufika mashine 150 ifikapo Desemba 2017 ambapo mashine hizo kila moja ina uwezo wa kupima wagonjwa 12 kwa siku na ifikapo Juni 2018 hospitali za Wilaya na Mikoa zitakuwa na mashine hizo zenye uwezo wa kutoa majibu ndani ya saa mbili.

No comments:

Post a Comment