Usiku huu katika Manispaa ya Bukoba kumetokea tetemeko. tetemeko hilo ambalo limetokea mida ya saa saba na nusu usiku huu wa kuamkia April 30, lilidumu kwa sekunde zisizozidi 15.
Mpaka sasa katika mitaa mbalimbali Watu wametoka nje ya nyumba zao wakiwa na aharuki kubwa na kuhofia tetemeko jingine.
Hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa mpaka sasa .
Kaa nasi tutaendelea kukupatia kinachojiri mkoani Kagera
No comments:
Post a Comment