Serikali imesema jumla ya
walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera,
wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048 kat ya nafasi 4,129
za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akizungumza
na Waandishi Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote
walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia
tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.
Amesema walimu walioajiriwa wamepangwa
moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina
upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.
Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada na walimu 1,544 ni wa Stashahada.
“Sehemu kubwa ya walimu wa
Shahada wamepangwa kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache
kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.
UPUNGUFU NI 60%
Simbachawene amekiri kuwa kuna upungufu
wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali
za sekondari nchini.
“Moja ya changamoto kubwa
ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa
walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo katika shule 3,602 ni
26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene
Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.
Amesema kwa sasa serikali ina shule za
sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na sita
huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .
Aidha amesema shule hizo za sekondari
kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo waliopo
ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.
“Kutokana na ziada hiyo ya
walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao
katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’
alisemaFUNGUA HAPA KUONA MAJINA YA WALIMU WA SHAHADA
FUNGUA HAPA KUONA MAJINA YA WALIOAJIRIWA
No comments:
Post a Comment