Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari.
Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao
"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki
Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.
"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma" -alisema Kairuki
No comments:
Post a Comment