SPIKA
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amemtumia Salam za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo kufuatia vifo vya Wananfunzi 29, Walimu 3 na
Dereva 1, wa Shule ya Msingi Lucky Vicent ya Mkoani Arusha, baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kupata ajali leo asubuhi katika eneo la Rhotia Marera, Wilayani Karatu
Mkoani Arusha.
“Mhe
Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya ajali iliyogharimu
maisha ya watoto wetu, hakika hili ni pigo kwa taifa zima, namuomba mungu
azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.” alisema Mheshimiwa Ndugai.
No comments:
Post a Comment