Azam ilishinda vita hiyo juzi baada ya kufanikiwa kuizidi ujanja Yanga kwa kutangulia kumtorosha Mbaraka katika kambi ya timu ya taifa na kuipiga bao Yanga ambayo ilitua katika kambi hiyo na kumkosa kinda huyo.
Mbaraka ambaye kabla ya kuitumikia Kagera msimu uliopita aliitumikia Simba amesaini mkataba huo wenye thamani ya sh 40 milioni akiacha sh 50 ml za Yanga waliotangulia kufanya naye mazungumzo mara mbili.
Awali mshambuliaji huyo aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi alitangulia kuonana na Yanga lakini uzembe wa mtendaji mmoja wa Yanga aliyeshindwa kumalizana na kinda huyo licha ya kukutana naye mara mbili kabla ya ligi kuisha ndiyo zilizoipa maumivu Yanga na kupokonywa tonge mdomoni.
Hata hivyo baadhi ya vigogo wa Yanga walipambana kumbadilisha akili kinda huyo lakini hatimaye Azam ikamnasa kupitia mtendaji wao mpya Abdul Mohamed na kumfanya kuwa mshambuliaji wa pili kusajiliwa akitanguliwa na Waziri Junior wa Toto ambaye naye alitangulia kuhitajiwa na Yanga kiasi cha kupiga picha na kombe la ligi la Yanga kisha kutua Azam jioni
No comments:
Post a Comment