Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wa Mambo ya Ndani Massauni amefunguka
na kusema hivi sasa madereva ambao watakuwa wakikiuka makosa ya
barabarani wanapaswa kuchukuliwa hatua kali ikiwezekana hata kuchalazwa
viboko.
Massauni amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya tathimini ya
utekelezaji wa mpango wa mkakati wa kupunguza ajali barabarani nchini
kwa asilimia 10 katika kipindi cha miezi sita kuanzia Agosti 2016 hadi
Januari 2017.
"Suala la kwanza tunataka kulipa kipaumbele ambalo hatukufanikiwa katika
mkakati wetu wa kwanza ni kuhusu NUKTA katika leseni za udereva
tulisema tuanze lakini hatukufanikiwa lakini suala la pili ni kuchukua
hatua kali dhidi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani,
ikibidi hata kuwachapa viboko maana lazima muda mwingine twende hivyo
hatua zitakuwa kali sana safari hii" alisema Massauni

No comments:
Post a Comment