MSHAMBULIAJI wa zamani wa Azam, John Raphael Bocco amesema hana hofu yoyote kuhusu ushindani wa namba uliopo ndani ya kikosi chao cha Simba, kwa sababu anaamini kwa wazawa hakuna straika anayeweza kumfikia kwenye kucheka na nyavu.
Bocco ambaye msimu ulioisha alifunga mabao tisa katika ligi kuu na kufanikiwa kushika nafasi ya saba kwenye orodha ya wafungaji bora licha ya kuwa majeruhi kwa mda mrefu, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.
Bocco amesema anaamini nafasi ya kuwa katika kikosi cha kwanza ipo kwa asilimia 99, kwa sababu washambuliaji aliowakuta wa kawaida sana na haoni wa kumfikia.
“Nimejipanga vizuri sana na ninaamini Simba ya msimu ujao itakuwa tishio kutokana na usajili uliofanywa kuwa mzuri na wenyewe malengo ya kuifikisha Simba mbali,” alisema Bocco.
Mbali na hayo, Bocco amesema maisha popote na pia anawashukuru viongozi wake wa zamani kwa kumjenga kisoka mpaka sasa alipofikia.
No comments:
Post a Comment