Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Saturday, June 24, 2017

LIONEL MESSI ASHEHEREKE SIKU YA KUZALIWA NA RECORD KIBAO ULAYA

Sijawahi kuona mpira ukitii mguu, lakini hakika mipira inatii miguu ya Lioneil Messi, uwezo wake uwanjani ni wa ajabu sana,jinsi anavyodrible mpira vinashangaza sana na ni kama game za Play Station.
Tuzo 5 za Ballon D’or, ni nani anaweza sogea mbele ya mfalme huyu na kama tuzo tu zilizotolewa na wazungu ambao hawana ujanja ujanja kama sisi zinasema Messi ni bora duniani mara tano, mimi ni nani haswa hadi niwabishie wao?
Magoli mengi ndani ya msimu mmoja, wanaocheza Ulaya wote ni mafundi na mabeki ni mabeki haswa na kuwapita inakubidi ufanye kazi haswa, lakini msimu wa mwaka 2011/2012 La Pulga aliweka kambani mabao 73 na hakuna aliyeweza kufunga idadi hii ya mabao katika msimu mmoja.
Mabao mengi El Classico, hakuna ubishi El Classico ni mchezo uliojaa ufundi sana na nguvu na hii inaufanya mchezo huu kuwa kati ya michezo migumi sana ulimwenguni, ila huu ni mgumu kwa wengine kwani La Pulga ameshapasia kamba mara 23 na hakuna aliyeweza kumzuia.
Mfungaji bora wa La Liga, ligi inayoitwa bora duniani na ligi iliyojaa mafundi ya Hispania, lakini unajua mfungaji wa kihistoria katika ligi hii? Si mwingine ni La Pulga ambaye hadi sasa kamba za La Liga ameshazifumania mara 349 ikiwa ni mara 64 zaidi ya Cristiano Ronaldo.
Mfungaji muda wote wa Barcelona, walipita kina Rivaldo kina Ronaldinho wakina Thiery Henry nao walikuwa bora sana lakini hakuna aliyeweza kugusa rekodi ya Messi kwani Muargentina huyo hadi sasa ameshaifungia Barcelona jumla ya mabao 538.
Assits nyingi katika La Liga, uzuri wa Messi tofauti na washambuliaji wengine ni kwamba sio mchoyo kwani huwa anafunga na kutoa assist, hadi sasa Lioneil Messi ametoa assists 137 katika ligi kuu nchini Hispania.
Mfungaji bora zaidi wa Argentina, japokuwa analaumiwa kutokuwa na kiwango kizuri katika timu ya taifa lakini Lioneil Messi ndio mshambuliaji anayeongoza kwa ufungaji katika timu ya taifa ya Argentina.
Mchezaji pekee kuwahi kufunga 40+ katika misimu 8 mfululizo. Ukitaja sifa za Lioneil Messi zote huwezi maliza kuandika, hakika ni nyingi mno na hakuna mchezaji katika dunia hii ameshawahi kufunga mabao zaidi ya 40 katila misimu 8 mfululizo.HAPPY 30 DAY LA PULGA


BOFYA HAPA KUPAKUA APPLICATION YETU 

No comments:

Post a Comment