Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Wednesday, June 28, 2017

NGOMA AWATOSA SIMBA AONGEZA MKATA YANGA



Mshambuliaji wa  Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Ngoma ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga waponzani wa Yanga, Simba kabla ya kuzuka kwa taarifa za kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi ya kuu ya Afrika Kusini 'Primiership ABS' ambapo alitua nchini usiku wa jana na  mchana  wa leo amesaini mkataba huo.

Ngoma aliwasili jana usiku Dar es Salaam baada ya taarifa kwamba amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Polokwane City ya Afrika Kusini.

Lakini tangu jana mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kabla ya leo mchana kusaini, hivyo pia kuzima tetesi za kwamba anataka kujiunga na mahasimu, Simba.

Katika miaka yake miwili ya kwanza, Ngoma alikuwa ana msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kuiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.

Na hata katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.

Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.

Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu. Na kwa kusaini Yanga, maana yake ataendelea kufanya kazi na rafiki zake, kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko na mshambuliaji Mzambia, Thabani Kamusoko

No comments:

Post a Comment