Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars imeanza vizuri michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA)
leo Jumapili kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi A kwenye Uwanja
wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
Mshambuliaji Ramadhani Shiza Kichuya
ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi katika mchezo huo baada ya kuonyesha
uwezo wa juu na kufanikiwa kufunga mabao yote ya mchezo huo katika dakika ya 13
na 18.
Ushindi huo umemfanya Kocha Salum Mayanga
kuandika ushindi wa tatu katika mechi nne tangu aanze kuifundisha Taifa Stars,
Machi, 2017 akichukua nafasi iliyoachwa na Charles Boniface Mkwasa.
Timu nyingine katika Kundi A mbali na
Tanzania na Malawi ni Mauritius na Angola wakati Kundi B lina timu za Msumbiji,
Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe.
Mshindi wa kwanza wa kila kundi
atakwenda moja kwa moja hatua ya Robo Fainali. Botswana, Zambia na Afrika
Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zimefuzu moja kwa moja robo fainali.
No comments:
Post a Comment