Aidha, watoto wenye mama mwenye elimu hufaulu zaidi kuliko wale wenye mama asiye na elimu na ufaulu huongezeka kulingana na kiwango cha elimu cha mama.
Baadhi ya Takwimu zinazotokana na tafiti mbalimbali kuhusu suala hili:
1. Afya ya mtoto inategemea sana na elimu ya mama
38% ya watoto (chini ya miaka 5) wenye mama asiye na elimu walipelekwa hospitali ndani ya siku 1 baada ya kupata homa ukilinganisha na 64% ya wale wenye mama mwenye elimu ya sekondari au zaidi.
2. Ufaulu wa watoto shuleni unategemea sana na kiwango cha elimu cha mama
Katika Utafiti wa Uwezo unaoangalia uwezo wa kujifunza wa watoto wa darasa la 1-3 iligundulika kuwa watoto wenye mama mwenye elimu walifaulu zaidi ya wale wenye mama asiye na elimu na ufaulu uliongezeka kulingana na kiwango cha elimu cha mama.
No comments:
Post a Comment