wapo wengine kabla ya kusajiliwa na timu wanazozihitaji hutoa masharti kwamba akifika klabuni ni lazima apewe jezi yenye namba anayoitaka, mfano mzuri ni Michael Ballack wakati anasajiliwa Chelsea alitaka namba 13 ambayo wakati huo ilikuwa inavaliwa na Gallas ambaye alikataa kubadilisha jezi matokeo yake ikalazimika kuondoka kumpisha Ballack aje avae jezi namba 13.
kwa upande wa mkenya Victor Wanyama, yeye alivyosajiliwa Celtic ya Scotland alichagua kuvaa jezi namba 67 ambayo ni namba kubwa, lakini alifanya hivyo makusudi kabisa na haikuwa bahati mbaya.
Kupitia Sports Extra ya Clouds FM, Wanya,ma ametaja sababu kubwa iliyomfanya aache namba nyingine zote na kuchagua namba 67 ambayo kiuhalisia ipo mbali sana.
“Kila mchezaji ana ndoto, kwa hiyo nilivyokwenda pale nikikuwa na ndoto na nilikuwa najua Celtic ni timu ambayo inashiriki Champions League halafu nilikuwa na ndoto siku moja niweze kushinda ubingwa wa Champions kitu ambacho bado sijafanikiwa lakini bado nina ndoto.”
“Nilifanya uchunguzi wangu nikagundua Celtic walishinda Champions League mwaka 1967 ndio maana nikamua kuvaa namba 67 ili iwe kumbukumbu kwangu nikiingia ndani nakumbuka mwaka wa mafanikio.”
Tangu alipo hamia Southampton Wanyama amekua akivaa jezi namba 12 hadi sasa Totenham anavaa jezi yenye namba 12 sambamba na akiwa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’.
No comments:
Post a Comment