Beki wa kati wa Simba Abdi Banda, amekamilisha mpago wake wa kujiunga na timu ya Baroka FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini maarufu kama ABSA, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Meneja wa mchezaji huyo Abduli Boznia, ameiambia Goal, kila kitu kimekwenda sawa na Banda, huenda asirudi Tanzania baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu ya taifa ya Taifa Stars, ambayo ipo nchini humo ikishiriki michuano ya COSAFA.
“Nikweli Banda amefanikiwa kupata timu ya kuchezea ambayo ni Boroka FC, ni timu nzuri ingawa inashika nafasi za chini kwenye msimamo anachotakiwa kukaza ili kuisaidia timu hiyo na yeye mwenye kuweza kujitangaza ili aweze kuonekana na timu nyingine,”amesema Boznia.
Kwaupande wake Banda amesema amefurahi kupata nafasi ya hiyo ya kucheza soka nje ya Tanzania na ameahidi kucheza kwa bidii ili aweze kufika mbali zaidi ya hapo Afrika Kusini.
Amesema anatambua changamoto anayokwenda kukutana nayo kwenye timu hiyo ya kuhakikisha anaipigania timu hiyo kuepuka kushuka daraja hivyo atajitahidi kuhakikisha anatimiza vyema majukumu yake na kuitangaza vyema Tanzania kwenye ligi hiyo maarufu Afrika.
“Naamini ndoto zangu zinaelekea kutimia kwani ilikuwa ni kilio changu cha siku nyingi kuona nacheza ligi ya ABSA, namshukuru pia Meneja wangu Bozinia kwa jitihada kubwa alizozifanya namimi namuahidi kutomuangusha katika muda ambao nitaichezea timu hiyo,”amesema Ajibu.
Banda anajiunga na Boroka FC, baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia Simba mwishoni mwa msimu uliopita ambao aliweza kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la FA, katika mchezo dhidi ya Mbao FC, ya Mwanza. 

SOURCE :GOAL.COM