TANGAZO LA KAZI ZA WADADISI (NAFASI 450)
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) inawatangazia watanzania wenye sifa kuomba
kazi ya muda ya udadisi au ukusanyaji wa takwimu nafasi 450 kwa ajili ya
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2017/18
(Household Budget Survey) utakaofanyika katika mikoa yote ya Tanzania
Bara. Utafiti huu unahitaji mwombaji atoke kwenye eneo ambalo utafiti
unafanyika na awe tayari kufanya kazi kwa kipindi chote cha miezi 12.
Sifa za mwombaji zinazohitajika pamoja na maeneo yaliyochaguliwa kwa
ajili ya utafiti huu yameanishwa kwenye tangazo la kazi ambalo
linapatikana kwenye kila Ofisi ya Mkoa ya Ofisi Taifa ya Takwimu.
Barua ya maombi ya kazi itumwe kwenye Ofisi ya NBS ya Mkoa ambako unaishi. Maombi yanatakiwa yatumwe kabla ya tarehe 12 Agosti, 2017
NB: i. Tangazo hili linapatikana kupitia www.nbs.go.tz pamoja na www.eastc.ac.tz
ii. Wale watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili ndio watakaoitwa. NBS haitahusika na gharama za kuja kwenye usaili huu.
IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MKUU
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
27 Julai, 2017
CLICK HERE FOR MORE INFORMATION

No comments:
Post a Comment