1. Ongeza mguso katika utu wako
Sketi na shati hufanya uonekane kikazi zaidi, kwa mvulana suruari na shati la mikono mirefu na tai haina shida. Inakufanya uonekane mwenye mvuto, usiweke marashi makali au vitu vya thamani mwilini kama saa ya bei ghali, heleni za dhahabu inamfanya mwajiri kuwa na wasiwasi na wewe namna gani atakulipa? kama maisha yako ni ghali kuliko mshahara wako?2. Angalia uvaaji
Upende au usipende, mwonekano wako unachangia namna ambavyo mwajiri atafanya maamuzi ya kukuajiri. Mtizamo unachangia kutokana na mwonekano wako, unaweza kuwa ni mtu ambaye una vigezo vyote kielimu lakini mwonekano wako usipokuwa mzuri utaathiri maamuzi ya kukuajiri. Hivyo unatakiwa kujua namna ya kuvaa kulingana na kazi unayoomba .3. Onyesha Umakini
Uvaaji wako unatakiwa umwonyeshe mwajiri au mtu anayekufanyia usaili kwamba unamaanisha kile unchoomba. Unatakiwa kuwa jasiri na mweledi. Hutatakiwi kuvaa suti, inategemea kazi gani unaomba ila unatakiwa upendeze. Usiende na mavazi ya kawaida kama Jeans na Tshirt. Ukienda umevaa kawaida mtu anayekyfanyia usaili unamwoshesha kwamba hata kazi unaweza kuichukulia kawaida. Unapovaa vizuri unaonyesha kujiheshimu na kuheshimu kazi unayoomba.4. Pangilia vitu vyako kwa umakini
Hakikisha nyaraka zinazohitajika ziko kwenye mpangilio unaofaa, ili unapozitoa zitoke kiutaratibu.5. Fanya Uchunguzi wako
Fuatilia kwa umakini na kujua mavazi yanayohitajika katika hiyo kazi, utamaduni wa hiyo kazi wakati unapoomba. Uchunguzi wako pia ujue viwango wanavyoviangalia katika uvaaji. Hata kama uvaaji wao ni wa kawaida, kwenye usaili usiende kawaida tu.Vitu vya kuepuka
Usivae sketi fupi, kujipondoa kuliko pitiliza au viatu virefu sana. Kwenye usaili sio sehemu ya maonyesho ya mavazi au manukato gani unatumia. Usivae nguo zenye rangi kali au za kung’aaa.Hata utakapo pata kazi endelea kuvaa vizuri, onesha mafanikio na uonekane unathamini na kujali kazi hivyo kwa namna unavyovaa. Kama unataka kupandishwa cheo vaa kama mwenye cheo hicho, usidharau umuhimu wa mavazi katika eneo lako la kazi.
No comments:
Post a Comment