Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa
vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali
maalum.
Taarifa
ya TCAA iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kuwa, kwa taasisi au
mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini
ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Tangazo
hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa
na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kupata picha
kutokea juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika
hasa yanapofanyika katika maeneo ya wazi.
Drones
zilitumika zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya
kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati
uliohudhuria.
No comments:
Post a Comment