BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA VYETI VYA WAHITIMU WA ASTASHAHADA NA
STASHAHADA KATIKA PROGRAMU ZA AFYA, MIFUGO NA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO
2015/2016
Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria
ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo
ya ufundi nchini.
NACTE ina
wajibu wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wenye sifa stahiki kwa mafunzo ya
programu za Afya, Mifugo na Ualimu yanayozingatia umahiri.
Baraza
linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa vyeti vya wahitimu wa mafunzo ya
programu za Afya, Mifugo na Ualimu wenye sifa stahiki kwa mwaka wa
masomo 2015/16 viko katika hatua za mwisho za uchapaji na vitatolewa
muda wowote ndani ya mwezi huu wa Julai 2017.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 14/07/2017
No comments:
Post a Comment