Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Wednesday, September 6, 2017

JOB VACANCIES AT MBEYA CITY COUNCIL

TANGAZO LA KAZI

06 September 2017


 TANGAZO LA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anayofuraha kutangaza nafasi 8 za ajira za kudumu za Watendaji wa Vijiji III na Dereva II nafasi 2 Ajira za Kudumu. Ajira hizo zinatokana na kibali cha Ajira kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kibali cha ajira mpya chenye Kumb. Na. FA170/364/01/41 cha tarehe 30 Julai, 2017 na Kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb. Na. CFC 26/205/01 “FF”/91 cha tarehe 22 Agosti.
DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2

1.1. KAZI ZA KUFANYA

Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
Kukusanya na kusambaza nyaraka Mbalimbali za Serikali.
Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri na usafi wakati wote na kufanya Uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari.
Kutunza na kuandika daftari la Safari “Log – book” kwa Safari zote.
Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wako

1.2. SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA

Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi daraja la II.
1.3.  MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya serikali yaani TGOS A1 yaani Tsh. 300.000/= kwa mwezi.

2. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 87

2.1. KAZI ZA KUFANYA 

Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
Kupokea, Kusikiliza na Kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za Kijiji.
Atawajibika kwa Mtendaji kata.
2.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA

Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2.3. MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali yaani TGS B1 yaani Tsh. 390,000/= kwa mwezi.
2.4. MASHARTI YA JUMLA 
Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wawe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela.
Maombi yote yaambatishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V)
Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya elimu (IV au VI), Ujuzi, cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni (Passport size) na iandikwe jina nyuma.
Testmonials”,”Provisional Results”,”Statement of results”, hati ya matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa UMMA hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kama wanakibali cha katibu Mkuu kiongozi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe  21.09.2017  saa 9.30 Alasiri.
Maombi yaandikwe kwa mkono na mwombaji mwenyewe na yatumwe Masijala ya Mkurugenzi Mtendaji (W) au kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
S.L.P 599,
MBEYA.

Imetolewa na:


Mkurugenzi Mtendaji (W)

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya