Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli anawatangazia wanchi wote wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kutuma maombi ya kazi kama ifuatavyo
1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 6
KAZI ZA KUFANYA
- kuendesha magari ya abiria namaroli
- Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri na usafi wakati wote na kufanya Uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
- Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari.
- Kutunza na kuandika daftari la Safari “Log – book” kwa Safari zote.
- kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi daraja la II.
umri kati ya miaka 18 - 40
1.3. MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya serikali yaani TGOS A 1
2. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 36
KAZI ZA KUFANYA
-Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
-Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
-Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- kusimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Kijiji
SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
umri
awe na umri kati ya miaka 18 - 40
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali yaani TGS B1
mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21/09/2017
maombi yote yatumwe kwa
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,
S.L.P 1,
Monduli.