Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka na kusema kuwa serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza mishahara ya wafanyakazi mwezi
huu Novemba kama Rais Magufuli alivyoagiza
Dkt.
Abbasi amesema hayo wakati akitoa tathmini ya miaka miwili ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli toka
alipoapishwa Novemba 5, 2015 na kusema kuanzia mwezi huu wafanyakazi
wataongezewa mishahara yao.
"Mwezi huu mishahara ya wafanyakazi wa Serikali itaongezwa kama Rais Magufuli alivyoahidi" Dkt. Hassan Abbasi
Mbali na hilo Msemaji wa Serikali amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli wameweza kufanikisha kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina pia amedai ndani ya muda huo Serikali imeanzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa.