TAARIFA KWA UMMA
Ninayo
furaha kuwatangazia wanachama , wapenzi , mashabiki na wadau wa Yanga
SC kuhusu makusanyo ya fedha za maendeleo ya klabu kutoka kwenu kwa
akaunti maalumu ya Selcom namba 150334.
Makusanyo
haya yanafanyika kupitia mitandao ya Mpesa , Tigo Pesa na Airtel Money .
Hakika mpaka sasa mwitikio ni mzuri na mimi kama katibu mkuu sambamba
na jopo zima la uongozi tunawashukuru sana wanachama wetu kwa moyo huu
mkubwa kwa timu yenu . Hakika tunajivunia ushirikiano wenu na tunawaomba
taarifa ya leo iwe chachu ya kufanya kikubwa zaidi ya hiki.
Ripoti
yetu inaanzia siku ya kwanza ya tarehe 24 April 2017 saa saba mchana (
13:00hrs ) tulipozindua harambee hii mpaka tarehe 27 April 2017 saa 7
mchana ( 13: 00 Hrs ) .
Makusanyo ;
1.24 April 2017 tulipokea entries 642 na jumla ya makusanyo ikawa 2 ,184,911.00
2. 25 April 2017 tulipokea entries 1181 na jumla ya makusanyo ikawa Tsh 4, 248,751.00
3. 26 April 2017 tulipokea entries 625 na jumla ya makusanyo ikawa Tsh 2,296,966.00
4. 27 April 2017 tulipokea entries 290 na jumla ya makusanyo ikawa Tsh 866,795.00
Jumla ya entries tulizopokea ni 2738 na kukusanya kiasi cha fedha cha Tsh milions 9 597 423.00/-
Mungu
awabariki sana . Kama uongozi tunasisitiza fedha hizi zitatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa baada ya kukusanywa . Lakini angalizo kwetu ;
ukiangalia tarehe na entries ( wachangiaji ) toka siku ya kwanza mpaka
jana inakwenda inashuka . Hii ina maana kwa kiasi fulani hamasa yetu
inapungua .
Tunawaomba
kwa pamoja tuhamasishane kupandisha makusanyo haya badala ya kushuka .
Kama tulivyochangia siku ya tarehe 25 April kiasi cha shilingi milioni 4
basi tusishuke chini ya hapo .
Mwisho
binafsi Boniface Mkwasa kama katibu mkuu wa klabu kwa niaba ya uongozi
tunawashukuru na kuwaomba ripoti hii iwe chachu ya kuchangia zaidi ili
juma lijalo nikitoa taarifa iwe zaidi ya hii. Kwa siku tatu kukusanya
shilingi milioni 9! toka kwenu hakika ni jambo kubwa.
Imetolewa na Idara ya habari na mawasiliano
Young african Sports Club
28.04.2017
No comments:
Post a Comment