Siku
moja baada ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kumshitaki kwa Kamati ya
Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi, ameibuka na kusema kesho hatofika
kusikiliza shitaka lake kwani ana majukumu ya timu yake.
Mkemi
alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kesho Jumapili katika Ofisi za
TFF saa 5 asubuhi baada ya kushutumiwa kwa kuidhalilisha Kamati ya Saa
72, kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika
kushughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji wa Kagera Sugar,
Mohammed Fakhi.
Mkemi
alisema: “Sitaweza kwenda kusikiliza nilichoitiwa katika siku hiyo ya
Jumapili kwani nipo Mwanza na timu na ndiyo kiongozi wa msafara.
“Tunacheza
na Mbao hiyo Jumapili hivyo nimeandika barua kwa TFF kuwataarifu kuwa
sitoweza kufika siku hiyo kama kamati ilivyonitaka hivyo wanipangie siku
nyingine.
“Mimi
sio mualifu isipokuwa ni tuhuma tu juu yangu hivyo ninatakapopangiwa
siku nyingine nitakwenda na wamekubali ombi langu hilo.”
Hata
hivyo, alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura simu yake
iliita bila kupokelewa. Juzi Wambura alitoa taarifa ya Mkemi kutakiwa
kwenda kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kuishambulia
Kamati ya Saa 72.
No comments:
Post a Comment