Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Saturday, May 6, 2017

ANDER HERRERA ATWAA TUZO MAN.UNITED AMBWAGA RASHFORD

KIUNGO Ander Herrera amechaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa klabu ya Manchester United baada ya kiiwango kizuri alichoonyesha.
Mspaniola huyo amepata asilimia 46 ya kura akimzidi Eric Bailly na Marcus Rashford ambao wote wamepata asilimia 27.
Herrera alikabidhiwa tuzo yake jana Uwanja wa mazoezi wa Aon Complex baada ya kuwasaidia Wekundu hao kushinda 1-0 nchini kwao, Hispania dhidi ya wenyeji Celta Vigo kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League.

Ander Herrera baada ya kukabidhiwa tuzo yake jana Uwanja wa mazoezi wa Aon Complex

Hii inakuwa mara ya tatu kiungo huyo anashinda tuzo hiyo, baada ya kushinda pia Februari na Aprili 2015.
Aliikosa kosa pia na tuzo ya Octoba mwaka jana baada ya kuzidiwa kidogo na Mspaniola mwenzake, Juan Mata.
Herrera amekuwa katika kiwango kizuri siku za karibuni kwenye Ligi Kuu ya England na zaidi aling'ara kwenye mchezo dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea.

No comments:

Post a Comment