Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Saturday, May 6, 2017

LOWASSA ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA ZA WAFIWA ARUSHA

Arusha. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva  wa gari hilo.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema

Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.

Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Tutaendelea kuwapa habari zaidi kuhusu tukio hili.

No comments:

Post a Comment