Mchezaji
wa timu ya SimbS SC, Mohamed Hussein "Tshabalala" amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu
wa 2016/2017.
Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa
Azam FC.
Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa
dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki
katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Pia alionesha nidhamu ya hali ya juu,hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.
Kwa kushinda tuzo hiyo,Hussein atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000
(milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Tanzania.
Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu
wa 2016/2017 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba
(Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda
(Novemba).
Wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera
Sugar (Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari),Mbaraka Yusuf wa
Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).
No comments:
Post a Comment