KLABU ya Arsenal haitaki kurudia makosa na sasa inataka kumsainisha mkataba mpya Aaron Ramsey mapema.
The
Gunners iliruhusu wachezaji wake kadhaa nyota kufikisha miezi 12 ya
mwisho kuelekea mwisho wa mikataba yao: Alexis Sanchez, Mesut Ozil, Alex
Oxlade-Chamberlain, Kieran Gibbs na Jack Wilshere wakiwa miongoni mwao
ambao wanaweza kuondoka bure Emirates msimu ujao.
Kwa
kushindwa kuwabana mapema kwa mikataba wachezaji hao, Arsenal inajiweka
kwenye mazingira ya kutumia fedha nyingi msimu ujao kusajili iwapo
nyota hao hata baadhi yao tu wataondoka bure.
Ndani
ya Uwanja wa Emirates hatua zimechukuliwa na uteuzi wa Huss Fahmy
katika uongozi kutoka timu ya Sky kushughulikia mikataba ni moja ya
mikakati ya kuhakikisha hilo halitokei.
Daniel
Levy hajaruhusu wachezaji wake kufika miaka miwili ya mwisho ya
mikataba yao kuhakikisha Tottenham haijiweki katika presha, na sasa The
Gunners wanafuata utaratibu huo.
Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu Ramsey, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2019, ni wa kwanza kuombwa asaini mkataba mpya.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Wales kwa sasa analipwa Pauni 100,000 kwa wiki na
katika mkataba mpya anatarajiwa kulipwa sawa na Ozil na Sanchez
wanaolipwa zaidi klabuni.
Danny
Welbeck, Theo Walcott na Petr Cech mikataba yao pia inamalizika mwaka
2019 na wanaweza kufuatia katika mazungumzo ya mikataba mipya.
No comments:
Post a Comment