WATANZANIA kwa mara
nyingine wamepata uhakika wa kushuhudia michuano mbalimbali mikubwa ya
kimataifa baada ya DStv Kupitia SuperSport kuingia makubaliano ya kurusha
michuano mikubwa ya kimataifa, ikiwemo michuano ya UEFA Euro 2020 pamoja na ile
ya kufuzu UEFA Euro 2020 na pia michuano
ya ulaya ya kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar.
Pia kuna lulu nyingine
kwa watazamaji wa DStv hasa washabiki wa kandanda kwani pia mashindano mapya ya
Ligi ya UEFA itakayoshindaniwa na timu kutoka nchi zote 55 ambazo ni wanachama
wa UEFA. Michuano hii pia itakuwa ikionyeshwa katika chaneli ya SuperSport.
Makubaliano haya
yanawahakikishia watazamaji wa DStv kushuhudia michuano yote mikubwa ya
soka kila msimu hadi mwaka 2022.
“UEFA inafurahi
kuendelea na kuimarisha uhusiano wake wa muda mrefu na supersport” amekaririwa
Guy-Laurent Epstein, Mkurugenzi Mtendaji wa
UEFA Events SA. “Supersport ni
mshirika wa miaka nenda rudi wa UEFA na tunaimani kubwa kuwa SuperSport
itaendelea kuwahakikishia watazamaji matangazo ya kiwango cha juu na pia amsha
amsha ya UEFA 2018-2022 kwa mamilioni ya
watazamaji wa mitandange hiyo barani Afrika – Kusini mwa jangwa la Sahara.
UEFA Euro 2020, ni moja
ya michuano itakayokuwa na shamrashamra nyingi ikizingatiwa kuwa itakuwa
inatimiza miaka 60 tangu kuanza kwa michuano hiyo. Michuano hiyo itafanyika
katika mini 13 ya nchi 13 tofauti barani Ulaya.
Michuano ya kufuzu ya
Ulaya (The European qualifiers) itakuwa ya aina yake wakati ambapo nchi 55
zitakabana koo kuwania nafasi 24 za kushiriki michuano hiyo. Michuano hii ya
kufuzu itaanza March 2019 hadi March 2020.
“Hii ni mikataba mikubwa
na muhimu sana” amesema Gideon Khobane, Afisa Mkuu wa SuperSport. “Michuano ya
ulaya kwa kawaida huwa na mvuto mkubwa sana kwa
watazamaji wetu hivyo kuyafanya moja ya mashindano muhimu sanan.
Tunaamini
kuwa michuano hii inaendelea kuwa mikubwa na maarufu Zaidi hivyo bila shaka
ushirikiano wa Supersport na UEFA utaongeza chachu katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment