Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua
uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia
leo tarehe 24 Mei, 2017.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya
Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.
Kutenguliwa kwa Prof Muhongo kumekuja saa chache baada ya Rais Magufuli kupokea taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa
nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Mara
baada ya kupokea ripoti hiyo Rais Magufuli alitangaza maamuzi
mbalimbali aliyoyachukua kutokana na taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na
kuvunja bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMMA) na
kumsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa TMMA ikiwa ni mapendekezo ya Kamati
hiyo.
Hii
ni mara ya pili kwa Prof Sospeter Muhongo kuondolewa katika Wizara
hiyo, baada ya Januari 24,2015 alipojiuzulu kufuatia shinikizo baada ya
kashfa ya Escrow, na Rais Magufuli alipoingia madarakani alimrejesha
katika wadhifa huo.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa
Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24
Mei, 2017.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Mei, 2017
No comments:
Post a Comment