Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison George Mwakyembe amevipiga marufuku vyombo vya habari nchini (runinga na redio) kusoma habari nzima zilizomo kwenye magazeti.Waziri Mwakyembe amesema kuwa marufuku hiyo inaanza kesho kwamba vyombo vya habari havitatakiwa kuisoma habari yote kama ilivyoandikwa kwenye gazeti.
Akieleza dhumuni la marufuku hii, Waziri Mwakyembe amesema ni ili magazeti yaweze kuuza kwani ukishasoma habari yote kwenye chombo cha habari na watu wakasiliza maelezo yote hakuna mtu atakayenunua gazeti hilo tena.Kauli hii ya waziri imekuja wakati dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi 3 katika orodha ya uhuru wa habari, hii ikichangiwa na uwepo wa sheria ya makosa ya mitandao, sheria ya huduma za habari pamoja na kutishwa, kujeruhiwa au kufungwa kwa waandishi wa habari.
Makamu
wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji,
akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, ambaye amemwakilisha Rais John Pombe Magufuli.
#BMGHabari
Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia), akizindua "Taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016". Kushoto ni mjumbe bodi ya Misa Tanzania, Lilian Lucas.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Uzinduzi wa "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment