Aliyekuwa
Waziri wa nishati na madini prof. Sospeter Muhongo, hajaonekana Bungeni
mjini Dodoma bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la
mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita .
Mei
24, mwaka huu, Ris John Mgufuli alitengua uteuzi wa prof. Muhongo
katika baraza la mawaziri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kukabidhiwa
ripoti ya kamati ya kwanza ya uchunguzi wa machanga wa dhahabu
(makinikia)
Mtaalamu
huyo wa jiolojia wa kimataifa hakuwapo bungeni wakati uteuzi wake wa
uwaziri ukitenguliwa, huku taarifa zikidai kuwa alirudi nyumbani kwao,
Musoma Mkoani Mara, kuhudhulia mazishi ya dada yake.
Katibu
wa bunge DK. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa ya
mbunge huyo wa Msoma Vijijini (CCM) jambo ambalo ni kinyume na
utaratibu.
Kiongozi huyo wa bunge pia alisema ofisi yake haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri mwishoni mwa mwezi uliopita
DK.
Kashililah aliongeza kuwa kwa kawaida mbunge anapokuwa na udhuru ,
humwandikia Spika kumuelezea hatakuwa bungeni kwa muda Fulani na ofisi
ya KAtibu wa Bunge hupewa nakala.
“Sijapata nakala yeyote ya udhuru, wa profesa Muhongo na wala sijui alipo tangu siku ile,” alisema DK. Kashililah.
Katibu
wa Bunge huyo alisema hii ni mara ya pili kwa Muhongo kuondoka Bungeni
kwa muda mrefu bila ya ruhusa kwani hata alipomwandikia barua ya
kujiuzulu Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, hakuhudhulia bunge kwa
muda mrefu.
No comments:
Post a Comment