Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.
Dk. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema kuwa wanaume wengi wamekuwa
vinara wa michepuko jambo ambalo linapelekea kupata virus vya UKIMWI na
kwenda kuwaambukiza wanawake.
Kigwangalla amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali lililoulizwa
na Mbunge wa Viti maalum CHADEMA, Susan Lyimo ambaye alitaka kujua
kwanini idadi kubwa ya wanawake ndiyo wamekuwa waathirika wa virus vya
UKIMWI, akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya alikiri kuwa ni kweli
kuna utofauti japo si mkubwa sana na kudai kuwa wanawake wengi wanapata
maambukizi haya kutokana na utofauti wa kibaolojia wa maumbile lakini
pia kutokana na mienendo ya wanawake na wanaume.
"Maambukizi kati ya wanawake na wanaume kuna uwiano, lakini hili la
wanawake kuwa wengi kuonekana wanapata virus vya UKIMWI ni kutokana na
utofauti ya kimaumbile ya kibaolojia kati ya wanawake na wanaume, tabia
za wanaume na wanawake. Lakini wanaume wengi wamekuwa na tabia za
kuchepuka sana hivyo wao wanaweza kuvitoa virus huko na kuleta kwa
wamama nyumbani, maana wanaume ndiyo chanzo cha michepuko ukilinganisha
na wanawake" alisema Kigwangalla
Mbali na hilo Kigwangalla aliwataka wanaume kuachana na tabia za
michepuko, na kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao na wenza wao ili
wame na uhakika na afya zao na kutopeleka virus hivyo kwa wake zao
majumbani kwao.
No comments:
Post a Comment