Uongozi
wa Yanga umempigia simu kiungo wake mshambuliaji, Deus Kaseke ukimtaka
arejee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya
kumuongezea mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo.
Kiungo
huyo, ni kati ya wachezaji 13 ambao mikataba yao imemalizika mwishoni
mwa msimu uliopita akiwemo Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Vincent
Bossou na Haruna Niyonzima anayetarajiwa kumwaga wino wakati wowote
Simba.
Awali,
kiungo huyo ilidaiwa kufuatwa na viongozi wa Simba kwa ajili ya kumpa
mkataba wa kuichezea timu hiyo kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Taarifa
za uhakika ni kuwa kiungo huyo anatarajiwa kutua Dar, leo kwa ndege
akitokea nyumbani kwao Mbeya alipokwenda kwa ajili ya mapumziko mara
baada ya ligi kuu kumalizika.
“Uongozi
umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao
imemalizika na kikubwa wanataka kuwaongezea mikataba mipya ya kuichezea
timu hiyo.
“Miongoni
mwa wachezaji hao ni Kaseke ambaye tayari uongozi umempigia simu na
kumuita Dar ili asaini aongeze mkataba na kesho (leo) anatarajiwa kutua
Dar kwa ndege kwa ajili ya kukamirisha usajili wake,” alisema mtoa
taarifa.
Alipotafutwa
Kaseke kuzungumzia hilo alisema: “Hizo taarifa za kweli, viongozi
wameniita kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine
mpya wa kuendelea kuichezea timu yangu hiyo na ndani ya wiki hii
nitakuwa tayari nimefika Dar.”
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema: “Uongozi hivi sasa upo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji tunaowahitaji ambao mikataba yao imemalizika, hivyo ni vema mkasubiria hadi tutakapokamilisha tutaweka wazi.
BOFYA HAPA UDOWNLOAD APPLICATION YETU PLAY STORE UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MOTO MOTO
No comments:
Post a Comment