Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Monday, July 3, 2017

BOCCO AONGEZWA KWENYE KIKOSI CHA STARS



Mshambuliaji mpya wa Simba, John Bocco ameongezwa katika kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo Afrika Kusini kwenye michuano ya COSAFA Castle.

Bocco ameongezwa katika kikosi hicho kufuatia mshambuliaji Mbaraka Yusuph kuumia.

Bocco ameitwa kwa ajili ya mechi ya kwanza ya kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Rwanda Julai 14 mjini Mwanza, kwa kuwa kwa sasa hataweza kuingizwa kwenye michuano ya COSAFA.

No comments:

Post a Comment