Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Monday, July 3, 2017

HUU HAPA UZI MPYA WA MANCHESTER UNITED



Klabu ya Manchester United imetambulisha jezi zake mpya ambazo itazitumia kwa mechi za nyumbani, kwenye msimu wa 2017/18.

Katika zoezi hilo la utambulishaji, mchezaji Wayne Rooney ni miongoni mwa wachezaji waliotumiwa na Kampuni ya Adidas kuvaa jezi hizo, japo mustakabali wa mwanandinga huyo kusalia klabuni hapo bado haujulikania.

Fulana za uzi huo wa kuvutia, zimewekwa vishikizo mpaka eneo la kooni.

Kwa mujibu wa Adidas, lengo la kuwekwa kwa vishikizo hivyo mpaka eneo la kooni, ni kujaribu kufananisha na jezi bora zilizo wahi kutumiwa na timu hiyo siku za nyuma.

Mbali na Rooney, wachezaji wengine waliotumika kwenye picha ya utambulisho, ni pamoja na Paul Pogba, David De Gea, Jesse Lingard, Luke Shaw na Phil Jones.

No comments:

Post a Comment