Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Wednesday, July 5, 2017

FANYA HAYA ILI KUJIOKOA MIKONONI MWA SIMBA MKALI

Ukikutana na simba ghafla, fanya haya..

Uwapo porini au sehemu yoyote ya wazi, halafu ghafla ukamwona simba (akiwa amekupa mgongo) na wakati yeye akiwa hajakuona na wakati huo ukijua kabisa muda wowote atakapogeuka anakuona, LALA CHALI au KIFUDIFUDI!

Simba atakapogeuka na kuona umelala, atakusogelea na kuanza kukugusa-gusa kwa miguu yake na masharubu. Jikaze tu usitikisike.Kwa kufanya hivyo, atafikiri wewe n mzoga, na simba halagi mzoga, anakula fresh kitu kinachotoa damu ya moto!

Atakaa hapo pembeni yako kwa muda kadhaa akiwa kama anakusubiria,we jikaze tu, usikohoe,kupiga chafya, kujigeuza au kucheka!

Baadae taratibu ataanza kuondoka zake, huyoooo...
Kwa jicho la wizi, unamcheck tu taratibu akiwa anatokomea,akishapotea mbali, unanyanyuka zako na kwenda zako nyumbani huku nguo yako ikiwa imelowana...

No comments:

Post a Comment