Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana tena leo Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambapo imejadili mgawanyiko katika Kamati ya uchaguzi ya TFF.
Walioondolewa kwenye kamati ya uchaguzi ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Domina Madeli, Omary Hamidu, Juma Lalika na Jeremia Wambura.
Sababu kubwa ya wajumbe hao kupigwa chini ni mvutano kwa baadhi ya wajumbe juu ya mambo mbalimbali katika mchakato mzima wa uchaguzi. Pia, kulikuwa na mgongano wa kimaslahi kutokana na mjumbe mmoja kuwa mjumbe pia wa kamati ya uchaguzi mkoa wa Kagera. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya awali Revocatus Kuuli anaendelea kuwa Mwenyekiti wa kamati mpya huku wajumbe wapya walioteuliwa ni pamoja na Mohammed Mchengelwa, Malangwe Mchungahela, Kiomoni Kibamba na Thadeus Karua
No comments:
Post a Comment