Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Tuesday, July 4, 2017

WATU KADHAA WAJERUHIWA KWA AJALI ASUBUHI HII



Watu kadhaa wanahofiwa kujeruhiwa baadhi ikiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria (daladala) kugongana na lori la Taka eneo la Ukonga Madafu jijini Dar es Salaam.

Daladala hilo lifanyalo safari zake kati ya Gongo la Mboto na Makumbusho liligongwa ubavuni kuanzia mlangoni na kusababisha majeruhi hao huku wengine wakihofiwa kufa, wakati daladala hilo likitaka kulipita gari lingine.

Baadhi ya Mashuda wamesema dereva wa daladala alikuwa akijaribu kulipita lori lingine ndipo akataka kugongana na klori hilo uso kwa uso na katika harakati za kulikwepa likagongwa ubavuni na kujeruhi watu.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi hapo baadae.

No comments:

Post a Comment