Breaking

PAKUA MCHAINA APP HAPA CHINI USOME HABARI ZETU HATA USIPOKUWA NA MB

Thursday, July 20, 2017

JO VOCANCY AT SERENGETI MUNICIPAL MUSOMA





Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti inatangaza nafasi (7) saba za ajira katika Kada ya Mhasibu Msaidizi (Assistant Accountant) kwa mshahara wa ngazi ya TGS B.

Sifa za muombaji:

1: Awe na cheti cha kufaulu mtihani mgumu wa uhasibu serikalini (Higher Standard Government Accauntancy Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa umma.
2: Awe na Stashahada (Diploma) ya kawaida yoyote kutoka Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikalini, uzoefu usiopungua mwaka (1) mmoja katika fani hiyo atafikiriwa kwanza.

Masharti ya Ajira:

1: Ajira hii ni ya mkataba wa mwaka (1) mmoja.
2: Mshahara utalipwa kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
3: Baada ya mkataba kuisha, atakayeonekana kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi ataongezewa muda wa mkataba mwingine.

Kutuma maombi:
Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) S.L.P 176 Mugumu-Serengeti.

Wakati wa kutuma maombi, watumaji wazingatie yafuatayo;
I/ Tuma barua ya maombi yenye anuani yako kamili, majina yako (3) matatu, Jina la Mdhamini wako na Anuani yake kamili, weka namba yako ya simu unayoitumia muda wote.
II/ Barua yako ya maombi iambatanishwe na nakala ya cheti cha taaluma yako na cheti cha kuhitimu kidato cha Nne (Form Four) au kidato cha Sita(Form Six) na Picha zako (Passport Size mbili).

Mwisho wa kupokea maombi ni 04, August 2017 Saa 9:30 Asubuhi, na usaili utafanyika 10, August 2017.

Imetolewa leo 20, July 2017 na;
Eng. Juma Hamsini,
Mkurugenzi Mtendaji (W) Serengeti.




No comments:

Post a Comment