TANGAZO LA KAZI ZA
WADADISI KATIKA MKOA WA MOROGORO.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) inawatangazia watanzania wenye sifa zilizoainishwa
hapo chini kuleta maombi yao ya kazi ya muda ya udadisi au ukusanyaji wa
takwimu kwa ajili ya Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2016/17. Utafiti huu unahitaji
mwombaji atoke kwenye mkoa ambao utafiti unafanyika.
Waombaji
wanatakiwa kuwa ni watanzania wenye sifa zifuatazo;
a) sifa
za msingi:-
i.
Umri wa miaka 18 na kuendelea,
ii.
Elimu ya kuanzia Kidato cha Nne,
iii.
Mkazi
kutoka katika Mkoa husika.
b) sifa
za ziada:-
i.
Elimu ya Cheti cha Ukusanyaji Takwimu rasmi
kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC),
ii.
Uzoefu
wa kazi ya kukusanya takwimu katika tafiti mbali mbali zilizofanywa na NBS,
iii.
Uzoefu
wa kufanya Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2014/15.
Barua
za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji akionesha anuani kamili na namba yake
ya simu pamoja na kuambatisha nakala ya vyeti vyote vya elimu na mafunzo, wasifu
wa mwombaji (CV).
Maombi
yatumwe kabla ya tarehe 09/09/2017 kwa kupitia anuani ifuatayo:
Meneja Takwimu wa Mkoa,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
S. L. P. 581
MOROGORO.
NB:
i. Tangazo hili linapatikana kupitia www.nbs.go.tz pamoja na www.eastc.ac.tz
ii. Wale watakaochaguliwa kwa
ajili ya usaili ndio watakaoitwa. NBS haitahusika na gharama za kuja kwenye usaili huu.
IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MKUU
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
24 August, 2017