Halmashauri ya Wilaya ya Wnanging'ombe ni moja kati ya hHalmashauri 6 zinazopatikana mkoa wa Njombe . makao yake makuu yapo katika kata ya Igwachanya . Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe inakua kwa kasi kiuchumi kutokana na kuboresha kwa shughuli za kiuchumi, mawasiliano na muingiliano wa sehemu kubwa ya uchumi hutegemea kilimo na mazao ya biashara kama vile maharage, miti, alizeti na viazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe anawatangazia Wananchi wote nafasi mbali mbali za kazi kwa watanzania wenyesifa kama ifuatavyo
1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NAFASI 52 –
SIFA ZA MUOMBAJI
- Mwombaji awe na elimu ya Diploma katika moja ya fani zifuatazo Utawala,Sheria,Elimu ya Jamii,Usimamizi wa fedha,Maendeleo ya Jamii,Na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
kwa kuzingatia viwango vya serikasli yaani TGS B
KAZI/MAJUKUMU
i. Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao na kuwa mlinzi wa amani katika mtaa
ii. katibu wa maendeleo ya mtaa
iii. Ataratibu na Kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
iv. Atakuwa Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
v. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
vi. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
vii. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika kijiji.
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
ix. Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji.
x. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
xi. Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji.
xii. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
xiii. Kazi nyingine zote atakazopangiwa na Mwajiri.
DEREVA DARAJA LA II NAFASI 2
SIFA ZA MUOMBAJI
- waombaji wawe na cheti cha mtihani wa kidato cha IV wenye leseni ya Daraja la C ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miatau bila kusababisha ajali, wenye cheti cha majaribio y aufundi Daraja la II kutoka vyuo vya udereva vinavyotambulika na serikali
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (basic army course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo VETA au chuo chochote kinachotambulika na serikali
NGAZI YA MSHAHARA
kwa kuzingatia viwango vya serikasli yaani TGOS A
KAZI NA MAJUKUMU
- kuendesha magari ya abiria na maroli
- kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo unaohitaji matengenezo
- kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari kugundua ubovu
- kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
- kutuna log - book kwa safari zote
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45
- barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa
- maombi yaambatane na maelezo binafsi anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika
- maombi yote yaambatanishwe na vyeti vya taaluma, melezo nakala za vyeti vya kidato cha 4 na 6 kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia kazi husika
- testimonials provisional results statement results na hati ya matokeo ya kidato cha 4 na 6 havitapokelewa
- waombaji waambatanishe picha moja ya hivi karibuni passportsize
- mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 8. 09. 2017 saa 9;30 Alasiri
maombi yote yatumwe kwa
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA ya WANGING'OMBE,
S.L.P 64.
NJOMBE